Pamoja na uongozi wa Azam Fc kusisitiza kuwa aliyekuwa mshambuliaji wao Ditram Nchimbi wamemuuza klabu ya Yanga, Polisi Tanzania ambayo alikuwa akiitumikia kwa mkopo imepeleka malalamiko TFF ikipinga uamuzi wa Azam kumuuza mchezaji huyo
Polisi Tanzania imedai kuwa kulikuwa na makubaliano baina yao na Azam Fc pamoja na Nchimbi kuwa alipaswa kubaki Polisi Tanzania kwa msimu mmoja
Aidha kwa upande wa Yanga wao hawana tatizo kwani wamefuata taratibu kumsajili Nchimbi ambaye kimsingi alikuwa ni mali ya Azam Fc na sio Polisi Tanzania
Azam Fc imemuuza Nchimbi kwenda Yanga kwa dau la usajili linalofikia Tsh Milioni 20. Mshambuliaji huyo alikuwa amebakisha mkataba wa miezi sita na klabu ya Azam Fc
Hivyo mgogoro uliopo unapaswa kumalizwa na Azam Fc, Polisi Tanzania na Nchimbi mwenyewe (kama alikuwa na makubaliano mengine na Polisi TZ)
Lakini pia, kama hautashughulikiwa kwa haraka, ni wazi inaweza kuwa sababu kwake kukosa mchezo dhidi ya Simba Januari 04 2020