Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amemlalamikia mwamuzi aliyechezesha mchezo wa ligi kuu leo dhidi ya Mbeya City kuwa alishindwa kutafsiri sheria 17 za soka
Mkwasa amesema mwamuzi huyo hakuitendea haki Yanga katika matukio mengi
"Kuna matukio yalitokea uwanjani ulisikia hata mashabiki wakipiga kelele. Kwa kweli ni aibu. Wakati mwingine hatupendi kuwalaumu waamuzi lakini wengine ni vichefuchefu," alisema Mkwasa
Katika mchezo huo mwamuzi Florentina Zablon alishindwa kuumudu ambapo moja ya matukio aliinyima Yanga mikwaju ya penati dhahiri
ADVERTISE HERE