Mbeya City wamekomaa, wapata sare dhidi ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Dec 2019
Mbeya City wamekomaa, wapata sare dhidi ya Yanga

Yanga imeshindwa kuondoka na alama zote tatu mkoani Mbeya baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine

Ni mchezo ambao haukuwa rahisi kwa kila timu kutokana na mazingira ya uwanja wa Sokoine

Mvua za rasharasha zilizonyesha muda mfupi kabla ya mchezo zilipelekea uwanja huo kujaa maji na tope na kusababisha mchezo kukosa ufundi

Ni matokeo ambayo sio mazuri kwa Yanga hasa ikizingatiwa michezo hii ya viporo wanapaswa kushinda ili kuwawea kwenye presha watani zao Simba ambao wako kileleni mwa msimamo wa ligi

Kimahesabu tayari Yanga imeacha alama nne kupitia michezo hiyo ya viporo ambapo hata ikishinda mingine iliyobaki itakuwa iko nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama nne

Hata hivyo ligi bado mbichi na mabingwa hao wa kihisoria wana nafasi ya kujisahihisha katika michezo inayokuja

Siku ya Ijumaa watarudi tena dimba la Sokoine kuumana na Tanzania Prisons

Mchezo huo pengine utakuwa mgumu zaidi kuliko mchezo waliocheza dhidi ya Mbeya City leo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’