Kikosi cha Yanga kinaendelea kusukwa upya dirisha dogo ili kuhakikisha mabingwa hao wa kihistoria wanarejesha umwamba wao uliopotea kwa misimu miwili sasa
Lakini pia maboresho hayo yamechagizwa na ujio wa mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao utapigwa January 04 2020 katika uwanja wa Taifa
Ukiangalia Yanga imeharakisha usajili wake ili kuhakikisha nyota wapya wanakuwa sehemu ya mchezo huo
Wanachokifanya mabosi wa Yanga sasa ni kupigania kupatikana kwa vibali vya nyota wao wa kigeni kwani kwa wachezaji wazawa hawana kikwazo
Nyota wa kigeni ambao watahitaji kupata vibali ili kuweza kushiriki mchezo huo ni Haruna Niyonzima ambaye usajili wake umekamilika na mshambuliaji raia wa Ivory Coast Yikpe Gnamien ambaye mchakato wake wa usajili unaelekea kukamilishwa
Ujio wa Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima, Tariq, Adeyum na Gnamien unakwenda kuibadili kabisa Yanga
Kocha Charles Mkwasa atakuwa na kikosi kipana, hakuna shaka atakuwa na timu imara zaidi
Nyota kama Nchimbi, Niyonzima na Adeyum wao wanatarajiwa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza
Pamoja na kuwa kwa sasa Yanga imeweka kipaumbele kwenye michezo mitatu ya viporo, ushindi katika mchezo wa Januari 04 ndio matokeo matamu zaidi ambayo mashabiki wanayasubiri
Hii ni kutokana na ukweli kuwa tangu mwaka 2015, Yanga haijanja radha ushindi dhidi ya watani zao Simba
Lakini baada ya maboresho hayo, kuna kila dalili kwa Yanga kurejesha umwamba wao katika michezo ya watani wa jadi kwani kwa takwimu za jumla Yanga imeshinda mechi nyingi zaidi ya Simba kwenye michezo inayozikutanisha timu hizo