Kikosi cha Yanga tayari kiko mkoani Mbeya ambako kesho Jumanne, Disemba 24 watashuka kwenye uwanja wa Sokoine kumenyana na Mbeya City
Kumekuwa na maswali baada ya wachezaji wanne waliokuwa timu ya Taifa ya Zanzibar kutojumuishwa kwenye kikosi hicho
Zanzibar iliondoshwa mapema kwenye michuano ya Chalenji hivyo ilitarajiwa wachezaji hao kuripoti kambini mapema tofauti na wenzao wa Bara
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema wachezaji hao walipewa mapumziko ya siku tatu baada ya kutoka Chalenji
Mapumziko yao yalimalizika juzi lakini kwa kuwa hawakufanya mazoezi na timu, kocha Charles Mkwasa ameamua kutowajumuisha katika kikosi chake
Aidha Nugaz amefafanua kuwa winga Mrisho Ngasa anauguliwa na mama yake wakati Juma Abdul na Kelvin Yondani wamepewa mapumziko kutokana na ushiriki wao kwenye michuano ya Chalenji