Kiungo mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amemkariisha nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amerejea rasmi Yanga
Sibomana ameeleza furaha yake kucheza pamoja na Niyonzima ambaye wanaitumikia pamoja timu ya Taifa ya Rwanda
"Nilikuwa na ndoto ya kucheza pamoja nawe katika timu moja. Nafurahi ndoto hiyo imetimia. Karibu tena kaka," ameandika Sibomana kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram
Niyonzima amereja rasmi Yanga, timu aliyoitumikia kwa misimu mitano kabla ya kusajiliwa na Simba mwaka 2017
ADVERTISE HERE