Keshokutwa Jumamosi, Disemba 21 2019 kikosi cha Yanga kitashuka uwanja wa Uhuru kuikaribisha Iringa United ukiwa ni mchezo wa kombe la FA raundi ya tatu
Yanga inayoendelea kusukwa upya kipindi hiki cha dirisha dogo, itakuwa na nafasi zaidi ya kushinda mchezo huo kuliko wapinzani wao
Kikosi cha kocha Charles Mkwasa kilikuwa mkoani Kigoma kwenye ziara maalum ambayo ilikuwa sehemu ya maandalizi ya mchezo huo
Yanga imeendelea kujifua uwanja wa Uhuru kuelekea mchezo huo
ADVERTISE HERE