Mshambuliaji Juma Balinya amesema pamoja na kuwa ameondoka Yanga, hatasahau ukarimu wa mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria
Balinya amesema akiwa Yanga alipitia changamoto mbalimbali ikiwemo la ukame wa mabao, lakini mashabiki walimvumilia na kumpa nafasi

"Sikuwa nimepata nafasi ya kuwashukuru mashabiki wa Yanga"
"Natumia nafasi hii kuwashukuru kwa ushirikiano mlionionyesha nyakati zote nilizopitia," ameandika Balinya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Pia nawashukuru viongozi pamoja na benchi la ufundi. Mimi ni binadamu, nawaomba radhi pale ambapo niliwakosea"
Balinya amerejea kwao Uganda baada ya makubaliano ya kuvunja mkataba wake na Yanga kufikiwa
Kwa sasa ni mchezaji huru na anaweza kujiunga na timu yoyote
ADVERTISE HERE