Ukitaja jina la Luis Miquissone kuna watu wanapatwa na presha hasa wakikumbuka kile alichokifanya mapema sana msimu huu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa
Sasa habari mbaya zaidi kwao ni kuwa mkali huyu anayecheza UD Songo kwa mkopo akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns, anakaribia kuvalishwa uzi wa njano na kijani
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Hassan Bumbuli ameweka dokezo hili..

Mpaka wakati huu, inaelezwa winga huyo mwenye kasi ya 'umeme' tayari yuko jijini Dar es salaam kukamilisha mazungumzo na mabingwa hao wa kihistoria
ADVERTISE HERE