Jana ilikuwa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa mshambuliaji David Molinga na beki Paulo Godfrey 'Boxer'
Ilikuwa siku ya furaha kwao kwani mlinda lango Ramadhani Kabwili na kikosi chake waliifanya vyema kazi yao!
Molinga ambaye tetesi nyingi ziliripotiwa kuwa anaondoka, yuko Kigoma akiendelea na majukumu yake na klabu ya Yanga
Pamoja nae ni Mrisho Ngasa ambaye juzi aliandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii ambao ulitafsiriwa vibaya kuwa alikuwa akiaga
Wachezaji hao huenda leo wakashuka dimbani mkoani Kigoma wakati Yanga itakapoikabili Mbao Fc kwenye mchezo wa kirafiki
ADVERTISE HERE