Lwandamina kufuta uteja kwa Omog?

Shabiki Waukweli By Shabiki Waukweli
β€’
18 Oct 2017
Lwandamina kufuta uteja kwa Omog?
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina anakaribia kutimiza mwaka mmoja katika kikosi cha Yanga alichoanza kukinoa mwezi Novemba 2016.

Katika msimu wake wa kwanza, Lwandamina alifanikiwa kuendeleza alipoishia Hans van Pluijm na kuiwezesha Yanga kutetea ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa tatu mfululizo.

Licha ya mafanikio yake ya kutwaa ubingwa katika kipindi kifupi, kocha Lwandamina bado ana mtihani wa kupata ushindi dhidi ya Simba.

Katika kipindi chake, Lwandamina amekutana na mpinzani wake Joseph Omog mara tatu na Yanga imepoteza katika michezo yote.

Mchezo wake wa kwanza dhidi ya Simba ilikuwa kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu na Simba ikashinda kwa mikwaju ya penati baada ya suluhu ya 0-0.

Akakutana na Simba kwenye mzunguuko wa pili katika ligi, Yanga ikachapwa mabao 2-1 Simba ikipata ushindi huku ikiwa na wachezaji 10 dimbani.

Ni August 23 walipokutana tena kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na Simba kushinda tena kwa mikwaju ya penati.

Timu hizo zinatarajia kukutana tena siku 10 zijazo, Oktoba 28 hiyo ikiwa ni mara ya nne kwa makocha Lwandamina na Omog.

Huku akiwa na kumbukumbu ya rekodi hiyo, kocha George Lwandamina amejipanga kufuta uteja dhidi ya Omog.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Zambia mahesabu yake yote ameyaelekeza kwenye mchezo huo wa Oktoba 28.

Kulidhihirisha hilo Lwandamina aliamua kuwaacha baadhi ya wachezaji wake muhimu kwenye safari ya kanda ya ziwa,

Wachezaji Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko, wameachwa katika safari hiyo ili waweze kupona kabisa majeraha yao.

Ngoma alitarajiwa kuungana na kikosi cha Yanga kitakachoivaa Stand United lakini hilo linaweza lisifanyike baada ya washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib kutimiza vyema majukumu yake.

Kamusoko na Tambwe wanatarajiwa kuwa fiti kabisa na kuwa tayari kutumika kwenye mchezo huo wa Oktoba 28 ambao Yanga inatarajiwa kuwa mwenyeji.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo dhidi ya Simba huku morali ya wachezaji ikiwa juu.

Aidha kurejea 'kimyakimya' kwa aliyekuwa Mwenyekiti wake Yusuph Maji kumechangia kuirudisha Yanga katika hali yake.

Manji akishirikiana na matajiri wengine ndani ya klabu ya Yanga wameweza kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawakabili wachezaji.

Ni juzi tu tumeshuhudia kwa mara ya kwanza msimu huu Yanga ikitumia usafiri wa ndege kwenda kanda ya ziwa.

Kwa upende wa wapinzani wao Simba, hali sio shwari hata kidogo.

Tambo zilizokuwa zinatolewa kuhusu ughali na ubora wa kikosi cha Simba zimeanza kuitafuna timu hiyo ambayo hivi karibuni imekuwa ikisaka ushindi kwa 'tochi'.

Kama ilivyokuwa kwa Yanga mwanzoni mwa msimu, Simba nayo inakabiliwa na majeruhi ya mara kwa mara kwa wachezaji wake muhimu.

Ukiacha majeruhi wa muda mrefu Shomari Kapombe na Said Mohammed 'Nduda', Simba itawakosa John Bocco na Salim Mbonde walioumia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kutaka kocha Mkuu Joseph Omog aondololewe licha ya ukweli kwamba kwa kiasi kikubwa kikosi cha Simba kimesajiliwa na viongozi wa timu hiyo bila kumshirikisha kocha.

Hiyo imepelekea Simba kuwa na wachezaji wengi wa aina moja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’