Mshambuliaji Tariq Seif Kiakala leo amesaini mkataba wa kuwatumikia mabingwa wa kihistoria, Yanga
Tariq alitua jana kutoka nchini Misri ambapo alipokelewa na Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Ruhago
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuzitumikia Biashara United na Stand United, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Yanga kuelekea dirisha dogo
Baada ya kusaini mkataba, anataweza kusajiliwa kwenye mfumo wa TFF kuanzia Disemba 16 siku ambayo dirisha dogo la usajili litafunguliwa
ADVERTISE HERE