Yanga yamuwinda Makambo kwa mkopo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Dec 2019
Yanga yamuwinda Makambo kwa mkopo

Uongozi wa Yanga unajaribu kumrejesha kwa mkopo aliyekuwa mshambuliaji wake Heritier Makambo ambaye anaitumikia Horoya Ac

Pamoja na jana kuifungia Horoya Ac moja ya mabao kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Nasr ukiwa mchezo wa kombe la Shirikisho, Makambo bado anakabiliwa na changamoto kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Horoya

Hata hivyo Mwinyi Zahera aliyekuwa kocha wa Yanga huenda akawa kikwazo kukamilishwa kwa dili hilo ambalo lingekamilika bila matatizo kama angekuwa bado ni mkufunzi wa Yanga

Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni, Zahera alisema Yanga itapaswa kumlipa Makambo mshahara wa Tsh Milioni 7 kwa mwezi kwani ndio pesa anayolipwa na Horoya

Yanga inahaha kuboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo mpaka sasa haijaonyesha makali ya kueleweka

Baada ya kuachana na mshambuliaji Sadnye Urikhob, mshambuliaji mwingine ambaye pia huenda akaachwa ni majeruhi Maybin Kalengo ambaye atarejesha klabu ya Zesco iliyokuwa imempeleka Yanga kwa mkopo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’