Balinya akana kuvunja mkataba Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Dec 2019
Balinya akana kuvunja mkataba Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amesema anarejea kwao Uganda kwa ajili ya mapumziko, atarudi kuendelea na majukumu yake Yanga

Mapema leo kulizagaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa baadhi ya nyota wa Yanga wamevunja mikataba yao wakieleza kuwa sababu ni madai ya mishahara

Balinya amesema yeye ni mwajiriwa wa Yanga kwa wale wanaodhani ameondoka klabuni wasubiri waone kama hatarudi

"Nimechoshwa na maswali yenu, mimi sijaajiriwa Uganda, nimeajiriwa Tanzania nikimaliza mapumziko nitarudi kuendelea na majukumu yangu," alisema

Balinya ni mmoja wa wachezaji wanne ambao mapema leo taarifa zilizagaa kuwa amevunja mkataba

Wengine ni Lamine Moro, Sadney Urikhob na David Molinga

Uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hizo na kusisitiza wachezaji wake wa kigeni wameondoka kwa kuwa wamepewa mapumziko maalum wakaone familia baada ya ligi kusimama

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’