Yanga inatarajiwa kufanya maboresho ya kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa katika kipindi cha siku 10 zijazo
Hakuna ubishi, upande wa beki wa kushoto inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwenye usajili huo
Kwa maneno rahisi ni kuwa Yanga kwa sasa haina beki wa kushoto wa asili, Jaffar Mohammed na Ally Mtoni wamelazimika kucheza kwa 'dharura' hasa baada ya Muharami Issa 'Marcelo' kushindwa kuwashawishi Zahera na hata Mkwasa
Jina la Erick Rutanga beki wa kushoto na nahodha wa Rayon Sport limetajwa sana kuwa yuko mbioni kutua Yanga
Yanga ilianza kumfuatilia Rutanga wakati wa usajili uliopita, mabosi wamedhamiria kuipata sahihi yake wakati huu
Lakini wapo Wanayanga ambao wanaamini pamoja na ujio wa Rutanga, mlinzi Haji Mwinyi Mngwali, nafasi yake ipo
Mwinyi aliachwa na kocha Mwinyi Zahera usajili uliopita, lakini bila shaka uamuzi huo aliufanya kimakosa
Kwani alimuacha Mwinyi akakosa mbadala wake huku Gadiel Michael akigoma kusaini mkataba mpya
Mwinyi alionyesha uwezo mzuri katika mechi za mwishoni mwa msimu uliopita wakati Gadiel akiwa majeruhi
Kwa sasa anaitumikia KMKM, ambayo alisaini mkataba wa miezi sita
Kama Yanga itaweza kumsajili Rutanga lakini pia ikamrejesha Haji Mwinyi, watakuwa wamemaliza kabisa changamoto ya upande wa kushoto