Lipuli Fc yawaita Yanga mezani, ni ishu ya Saliboko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Dec 2019
Lipuli Fc yawaita Yanga mezani, ni ishu ya Saliboko

Klabu ya Yanga inahusishwa kumuwania mshambuliaji wa Lipuli Fc Daruweshi Saliboko ambaye wanamuwinda ili kumuongeza wakati wa usajili wa dirisha dogo

Tangu wiki iliyopita zimeripotiwa taarifa za nyota huyo aliyeifungia Lipuli Fc mabao sita kwenye ligi msimu huu kuingia kwenye rada za Yanga

Hata hivyo uongozi wa Lipuli umesema hakuna mazungumzo yoyote kati yao na Yanga lakini wako tayari kufanya mazungumzo na Yanga au timu yoyote inayomtaka Saliboko

Mwenyekiti wa Lipuli FC, Ayoub Kihwelo, amesema kama kuna timu inamuhitaji mchezaji huyo ni muhimu ikafuata taratibu zinazotakiwa.

"Taarifa ya mchezaji wetu kutakiwa na Yanga tunaisikia tu, lakini hakuna ofa tuliyopokea, kama wanamtaka tunawakaribisha mezani," alisema

Yanga inatarajiwa kufanya maboresho ya kikosi chake wakati wa usajili wa dirisha dogo utakaofunguliwa Disemba 16 mpaka Januari 15 2020

Juzi baada ya mchezo dhidi ya KMC ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, Kaimu kocha mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ina maoungufu, watatumia dirisha dogo kujiimarisha

Saliboko bado ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Lipuli Fc

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’