Mahesabu makali ya Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Oct 2017
Mahesabu makali ya Lwandamina
Baada ya Yanga kufikisha alama 12, kuwa sawa na Simba, Azam na Mtibwa Sugar, kocha Mkuu wa timu hiyo George Lwandamina amesema kazi iliyobaki ni kuhakikisha Yanga inaendelea kubaki nafasi za juu hadi kutwaa ubingwa.

Yanga ilianza msimu taratibu amapo kwenye mchezo wa ufunguzi ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Lipuli kabla ya kupata ushindi mwembamba dhidi ya Njombe Mji.

Baadae ikalazimishwa sare na Majimaji kisha ikapata ushindi mwembamba dhidi ya Ndanda kabla haijalazimishwa sare ya Mtibwa Sugar.

Wikiendi iliyopita Yanga ilizinduka na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Lwandamina amesema mwenendo wa timu mwanzoni mwa msimu haukuwa mzuri kutokana na changamoto ya majeruhi iliyoikabili timu yake.

Yanga imekuwa ikisumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara ambapo mpaka sasa bado Yanga imeshindwa kumtumia kabisa Amissi Tambwe ambaye ametonesha tena majeraha yake.

Donald Ngoma anaweza kurejea kwenye mchezo dhidi ya Stand United wakati Thabani Kamusoko huenda akarejea dimbani katika mchezo dhidi ya Simba, Oktoba 28.

Kocha huyo asiye na maneno mengi amedokeza kuwa huenda akalazimika kuongeza wachezaji wapya dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa siku 30 zijazo.

Ukiacha nafasi ya beki wa kati ambayo tayari Mcongomani Fiston Kayembe atasajiliwa, Yanga pia huenda ikasajili mshambuliaji wa kati atakayechukua nafasi ya Amissi Tambwe kama hali yake haitaimarika.

Pia Yanga inasaka winga wa kulia mwenye umahiri atakayeziba pengo la Simon Msuva baada ya wote waliosajiliwa kushindwa jukumu hilo.

Kinyume na ilivyotarajiwa, sasa Yanga inamtumia kiungo Pius Buswita kucheza winga ya kulia na anastahili pongezi kwani amecheza vizuri katika michezo aliyopangwa nafasi hiyo.

Kwa miaka mingi, Yanga imekuwa ikifanikiwa zaidi kwa kutumia washambuliaji wa pembeni. Msimu huu umekuwa mgumu baada ya Msuva kuondoka.

Ikumbukwe pia Yanga inakabiliwa na michuano ya klabu bingwa barani Afrika hivyo ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo ni vizuri mapungufu yaliyojitokeza yakafanyiwa kazi mapema.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
46m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’