Ratiba haikuwa rafiki kwetu - Mkwasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2019
Ratiba haikuwa rafiki kwetu - Mkwasa

Pamoja na kukubali matokeo baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi kuu, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema ratiba imechangia timu yake kutofanya vizuri leo

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, Mkwasa amelalamika kuwa ratiba haikuwa rafiki kwao

"Tumecheza Ijumaa Mwanza halafu Jumatatu tunacheza Dar es salaam. Wachezaji wangu leo hawakuwa katika ubora wao kutokana na uchovu," amesema

"Hata hivyo nawapongeza KMC kwa kutupa changamoto, wamecheza vizuri"

Mkwasa amesema bado timu yake ina changamoto hasa katika safu ya ushambuliaji, amesema watatumia dirisha dogo kurekebisha tatizo hilo

"Bado tuna kazi ya kufanya, safu yetu ya ushambuliaji bado inashindwa kutumia nafasi nyingi tunazotengeneza. Kuelekea dirisha dogo nadhani tutakuwa na nafasi ya kufanya maboresho"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’