Msimu uliopita KMC ilikutana na Yanga mara mbili kwenye ligi kuu na ilifungwa michezo yote
Mchezo wa duru la kwanza Yanga ilishinda kwa bao 1-0, bao la dakika za usiku lililowekwa kimiani kwa mpira wa dhabu wa Feisal Salum 'Fei Toto'
Mchezo wa pili Yanga ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1, mlinzi Ally Ally wakati huo akiwa KMC, alifunga bao la kichwa katika jitihada za kuokoa krosi iliyochongwa na Ibrahim Ajib (sasa yuko Simba)
Wakati Yanga ikiwa 'on-fire' baada ya kushinda michezo mitano mfululizo, KMC imekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu ikifanikiwa kushinda michezo miwili tu mpaka sasa
Kama ilivyo kwa Yanga, KMC nao walimtimua kocha wao Jackson Mayanja hivi karibuni
Lakini bado timu hiyo imeendelea kuchezea vichapo katika michezo yao
Pamoja na mazingira hayo, bado mchezo huo hautakuwa mwepesi kwa Yanga
Kwani kwa timu yoyote inayokutana na Yanga, mchezo unakuwa kama fainali kwao
Ushindi kwa Yanga utawahakikishia mabingwa hao wa kihistoria kuchupa hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 12 ambayo wapo sasa