Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mapinduzi Balama amerejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua
Balama leo alishiriki mazoezi ya mwisho ya Yanga yaliyofanyika uwanja wa Taifa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Kiungo huyo mnyumbufu alikosa mchezo uliopita dhidi ya waajiri wake wa zamani, Alliance FC
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa huenda akamrejesha moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya KMC
ADVERTISE HERE