Uvumilivu wamrejesha Abdul Stars

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
1 Dec 2019
Uvumilivu wamrejesha Abdul Stars

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul ni miongoni mwa wachezaji 32 walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije kuunda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' ambayo itashiriki michuano ya CECAFA Senior Challenge itakayofanyika nchini Uganda kuanzia Disemba 07

Abdul amerejea kikosi cha Stars baada ya kupita kipindi kigumu cha majeruhi na kukosa nafasi kikosi cha kwanza

Msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kutokana na majeraha yaliyopelekea kupoteza nafasi yake kwa kinda Paulo Godfrey 'Boxer' ambaye alipandishwa kikosi cha kwanza na aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera

Pamoja na changamoto zote, Abdul hakukata tamaa, alionyesha uvumilivu huku akijituma kuonyesha uwezo kila alipopewa nafasi

Ni uvumilivu wake huo ambao ulimuwezesha kurejea kikosi cha kwanza Yanga baada ya Boxer kuumia pamoja na presha ya mashabiki ambao walimshinikiza Zahera amchezeshe

Katika mechi za karibuni Abdul ameanza kuonyesha makali aliyokuwa nayo misimu miwili iliyopita

Kuitwa kwake Stars ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya dimbani sasa

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’