Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema pamoja na timu yake kupata ushindi katika mechi zote tatu za kwanza, bado hajaridhika na idadi ya mabao wanayofunga
Mkwasa ameweka mkazo katika safu yake ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanatumia vyema nafasi nyingi wanazotengeneza
"Ni jambo la faraja kuona timu imeendelea kuimarika, lakini bado tuna kazi ya kufanya"
"Tunapaswa kuongeza umakini na kutumia vyema nafasi nyingi tunazotengeneza," alisema Mkwasa baada ya mazoezi yaliyofanyika chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam jana
Mkwasa ameweka nguvu kubwa katika kuboresha safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu akabidhiwe majukumu ya kuinoa Yanga mapema mwezi huu, mafanikio yameanza kuonekana
Chini ya Mkwasa, Yanga imefunga mabao sita na kuruhusu mabao matatu katika mechi tatu walizocheza mpaka sasa
Kabla ya Mkwasa, Yanga ilifunga mabao matano na kuruhusu mabao manne ndani ya mechi nne
Hata hivyo kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa bado ana kazi nyingine ya kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imeendelea kuruhusu mabao, wastani wa bao moja kila mchezo