Mzunguuko wa sita ligi ya Vodacom umekamilika leo kwa michezo miwili kupigwa jijini Dar es Salaam na mkoani Mbeya.
Katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, Simba imeponea chupuchupu kuaibishwa na Mtibwa Sugar baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1, Simba ikisawazisha dakika ya mwisho kabisa.
Tanzania Prisons imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Stand United.
Katika mzunguuko wote wa sita hakuna timu iliyoibuka na ushindi zaidi ya Yanga ambayo iliilaza Kagera Sugar mabao 2-1.
Hakuna mshindi katika viwanja vingine saba.
Simba imerejea kileleni kwa tofauti ya mabao baada ya kufikisha alama 12 sawa na Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC.
Yanga na Mtibwa Sugar zina takwimu sawa! Kwa maana hiyo, Mtibwa inakuwa ya pili kwa sababu ya herufi yake ya mwanzo kutangulia.
Baada ya mzunguuko wa sita kukamilika unaweza kupata picha jinsi ligi ya msimu huu ilivyongumu.
Wale waliokuwa wanadhani msimu huu ni 'kupiga tu' kila timu utakayokutana nayo waamke kutoka ndotoni!

ADVERTISE HERE