Yanga yasaka alama tatu muhimu dhidi ya Alliance Fc leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2019
Yanga yasaka alama tatu muhimu dhidi ya Alliance Fc leo

Kikosi cha Yanga leo Ijumaa saa kumi jioni kitashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Alliance Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu

Yanga iko jijini Mwanza tangu juzi ikijiandaa na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Mwanza na maeneo ya jirani

Hii itakuwa mara ya nne Yanga kukutana na Alliance Fc ambapo mabingwa hao wa kihistoria walishinda michezo yote mitatu waliyocheza msimu uliopita

Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiwekea mazingira mazuri ya kuurejesha ubingwa wa ligi kuu ambao uko mikononi kwa watani zao Simba kwa misimu miwili sasa

Hata hivyo mchezo hautakuwa mwepesi kwani Alliance Fc imeonekana kuimarika sana msimu huu

Aidha kipigo cha mabao 5-0 walichokipata kwenye mchezo uliopita kutoka kwa Azam Fc, kinawafanya watoto hao wa shule wawe na shauku ya kufanya vizuri leo

Kaimu kocha mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema wamejipanga kuondoka na alama zote tatu

Yanga itarejea jijini Dar es salaam leo baada ya mchezo huo kwani Jumatatu inakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya KMC ambao utapigwa uwanja wa Uhuru

Β 

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’