Yanga kuchangia damu Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2019
Yanga kuchangia damu Mwanza

Kesho Ijumaa Novemba 29 2019, mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga watashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kumenyana na Alliance Fc katika mchezo wa ligi kuu

Lakini mapema kabla ya mchezo huo, Wanachama wa klabu ya Yanga mkoani Mwanza watashiriki shughuli za kijamii

Afisa Mhamasishaji na Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz, amesema saa tatu asubuhi Wanachama wa timu hiyo wapatao 200 watachangia damu Hospitali ya Bugando

Pia watatoa sukari na taulo za kujihifadhi kwa ajili ya kinamama waliojifungua na wanawake wengine wenye uhitaji Hospitalini hapo

"Yanga ni timu ya Mwananchi. Hivyo kesho kabla ya mchezo wetu dhidi ya Alliance, tutajitoa kwa ajili ya Wananchi. Wanachama wapatao 200 jijini Mwanza watachangia damu Hospitali ya Bugando pamoja na kutoa misaada mingine kama kugawa sukari kilo 200 na taulo za kujihifadhi kwa ajili ya kina mama zetu waliojifungua na wengine wenye mahitaji," amesema

Baada ya matukio hayo Nugaz amesema jioni Wanayanga wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuiunga mkono timu yao

Amesema kama ilivyo kawaida ya GSM, kitita cha Tsh Milioni 10 kitatolewa kwa Yanga kama itashinda mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
23h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’