Yanga yafafanua Bui, Feisal, Banka kuikosa Alliance Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Nov 2019
Yanga yafafanua Bui, Feisal, Banka kuikosa Alliance Fc

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema viungo Abdulaziz Makame, Feisal Salum na Mohammed Issa hawajajumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichosafiri jijini Mwanza kwa kuwa tayari wamejiunga na timu ya Taifa ya Zanzibar iliyoanza maandalizi ya michuano ya Chalenji

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Bumbuli alisema walipata taarifa ya mechi dhidi ya Alliance Fc na KMC wakiwa tayari wameshawapa ruhusa wachezaji hao

"Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania tuliwarusu kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Zanzibar. Lakini baadae tukapewa taarifa kuwa tunapaswa kucheza na Alliance na KMC," alisema Bumbuli

"Kutokana na udharura huo uliotokea, viongozi wameona ni busara tusiwasumbue kwa kuwa tunao wachezaji wengine wa kucheza nafasi zao"

"Benchi la ufundi wametuhakikishia kuwa kikosi kiko imara kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Alliance"

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo mwingine dhidi ya KMC utakaopigwa Jumatatu, Disemba 02 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
59m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’