Wachezaji Yanga wakabiliana na baridi Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Nov 2019
Wachezaji Yanga wakabiliana na baridi Mwanza

Daktari wa kikosi cha Yanga Dk Sheki Mgazija amesema timu inaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa Ijumaa, Novemba 29

Akizungumza kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyikwa uwanja wa Chuo cha Ualimu Butimba, Mgazija amesema hali ya hewa ya jiji la Mwanza ni baridi

Hivyo amesema benchi la ufundi linawapa wachezaji mazoezi maalum kuhakikisha wanazoea hali hiyo haraka

"Timu imefika salama, wachezaji wote wako kwenye hali nzuri leo tumeanza maandalizi kuelekea mchezo wa keshokutwa," amesema

"Hali ya hewa hapa Mwanza ni baridi tofauti Dar es salaam, benchi la ufundi linafanya kazi kuhakikisha wachezaji wanazoea hali hii haraka"

Baada ya kuwasili jijini Mwanza mapema leo, Yanga haikupoteza muda ambapo jioni imefanya mazoezi uwanja huo wa Butimba

Kesho Alhamisi mabingwa hao wa kihistoria watajifua kwenye uwanja wa CCM Kirumba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’