Yanga yatua Mwanza, kujifua chuoni Butimba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Nov 2019
Yanga yatua Mwanza, kujifua chuoni Butimba

Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga kimewasili jijini Mwanza tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Alliance utakaopigwa Ijumaa katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Timu hizo zinatarajia kukutana kwa mara ya nne huku Yanga ikijivunia ushindi katika mechi tatu, hivyo mchezo huo utakuwa wa kuvunja au kuendeleza rekodi.

Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa ameeleza kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao kutopata matokeo mazuri katika mchezo wao uliopita.

Jana Alliance Fc ilifumuliwa mabao 5-0 na Azam Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Nyagana

Ameongeza kuwa ishu ya uwanja utakaotumika, anaufahamu vizuri kwani ameuchezea hivyo haumpi wasiwasi na kwamba wamejipanga kushinda.

"Siwezi kueleza mipango kwa undani ila tumejipanga kushinda, tunajua tutapata changamoto kwasababu wapinzani kupata matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi yao iliyopita, ishu ya uwanja hainipi wasiwasi naujua vizuri," Mkwasa amenukuliwa na Mwanaspoti

Aidha baada ya kuwasili kwa timu hiyo imeelezwa huenda leo Jumatano ikajifua kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Butimba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’