Ushauri wa bure kwa viongozi wa Yanga

Admin By Admin
β€’
27 Jun 2017
Ushauri wa bure kwa viongozi wa Yanga
Klabu ya Yanga inahaha kuwabakisha baadhi ya wachezaji wake muhimu waliomaliza mikataba yao. Taarifa tulizonazo kuna takribani wachezaji 13 kwenye kikosi cha Yanga ambao wamemaliza mikataba.

Hili si jambo jema hata kidogo kufika mwishoni mwa msimu na idadi kubwa kama hiyo ya wachazaji wasio na mikataba.

Yanga iwe na utaratibu wa kuhuisha mikataba ya wachezaji wake mapema hata mwaka au wakichelewa sana miezi sita kabla mkataba wa mchezaji ambaye anahitajika haujamalizika kama tunavyoona ligi za Ulaya.

Kwani kipindi hiki cha usajili wanalazimika kutumia pesa nyingi kuwasajili wachezaji wao wenyewe wakati wangewapa mikataba mapema isingekuwa hivyo.

Leo hii wachezaji kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Deo Munishi, Deus Kaseke, Vicent Bossou, Oscar Joshua na wengineo mikataba yao imemalizika wakati baadhi yao ni wachezaji wa kutegemewa.

Yanga ingewapa mikataba mapema leo hii isingekuwa inapambana na Simba kuwagombea akina Haruna Niyonzima, Donald Ngoma na wengine ambao Simba iko tayari kuwanunua ili mradi tu kuvuruga kikosi cha Yanga.

Simba imekuwa huru kusajili wachezaji wengi wapya kwa kuwa wachezaji wake muhimu wengi walikuwa na mikataba iliyo hai.

Wachezaji waliomaliza mikataba Simba hawazidi watano na ukiacha Ajib aliyegoma kusaini mkataba mpya wengine wameongeza mikataba yao.

Natumai Katibu Mkuu Charles Mkwassa atalifanyia kazi hili na kupata suluhu ya kudumu ili wakati dirisha la usajili likifunguliwa kama hivi basi timu haipati kazi kuboresha kikosi.

Kwani sasa kama wacheaji wote ambao mikataba yao imekwisha watagoma kusaini mikataba mipya timu italazimika kusajili zaidi ya wachezaji 13 jambo ambalo sio zuri.

Kusajili kikosi kipya kuna gharama yake kwani wachezaji wapya huhitaji muda wa kuzoeana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’