Kesho Jumatano, Novemba 27 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, amesema timu inaekea Mwanza ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo
"Wachezaji wamerejea mazoezi leo (jana) baada ya mapumziko ya siku nne. Mwalimu alitoa mapumziko kwa sababu awali ratiba yetu haikuwa ikionyesha kuwa tunapaswa kucheza Novemba 29," alisema
"Pamoja na kuwa wametushtukiza lakini tumejipanga vizuri kushinda mchezo huo jijini Mwanza"
Baada ya mchezo huo, Yanga huenda ikashuka tena dimbani Disemba 02 kuikabili KMC ukiwa pia ni mchezo wa kiporo
ADVERTISE HERE