Mkwasa agoma kulinganishwa na Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Nov 2019
Mkwasa agoma kulinganishwa na Zahera

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amezidi kuwapa mzuka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo baada ya Ijumaa kupata ushindi dhidi ya JKT Tanzania, lakini kocha huyo amefunguka akitaka asifananishwe kabisa na mtangulizi wake, Mwinyi Zahera.

Mkwasa tangu akabidhiwe Yanga baada ya Zahera kufurushwa Jangwani, timu yake imeshinda mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara ikiwamo ile ya 1-0 dhidi ya Ndanda na ya juzi kuwafumua JKT kwa mabao 3-2 na mashabiki wakipigia chapuo akabidhiwe timu jumla kwa kubadilika kwa kikosi.

Kocha huyo, alifichua mabadiliko hayo yamekuja kupitia mazoezi ambayo anawapa wachezaji wake na kutaka asilinganishwe kwa kila anachokifanya kwa kutazamwa na yale ya Zahera.

"Kila mtu anaona kabisa namna tunavyocheza, huko nyuma mnajua walivyokuwa wanacheza na watu wanasema hivyo bado najaribu kuweka timu iwe sawa na muunganiko mzuri," alisema.

Mkwasa aliongeza kwa kusema licha ya kwamba wanapata matokeo, bado anaendelea kukisuka kikosi hiko ili kiweze kuwa bora zaidi msimu huu.

"Bado najenga timu mpaka hivi sasa, kwa mfano ukiangalia Makame alikuwa yupo Taifa Stars na alirejea tukiwa tuna muda mchache kuja katika mechi hii, nilimpa muda wa kupumzika na kunyoosha misuli, sikumpanga kwani hakuwepo na hajui tulikuwa tunafanya nini ndio maana akaingia kipindi cha pili"

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’