Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru leo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Mchezo huo utapigwa saa kumi jioni viingilio vikiwa; VIP Tsh 10,000/- na Mzunguuko Tsh 5,000/-
Ikiwa chini ya Boniface Mkwasa, Yanga imepania kuendeleza wimbi la ushindi leo dhidi ya timu ngumu ya JKT Tanzania
Msimu uliopita Yanga iliweza kushinda mechi zote mbili dhidi ya JKT Tanzania
Ilianza kwa kushinda mabao 3-0 na baadae kushinda 1-0 katika mchezo wa pili
Ushindi katika mchezo wa leo utaifanya Yanga ifikishe alama 13 na kuendelea kusogea juu katika msimamo wa ligi
Kimahesabu Yanga inaweza kuzifika alama ambazo wanazo vinara wa ligi hiyo Simba, kama watashinda mechi zao zote za viporo
Hii ni sababu ya Yanga kushinda kila mchezo ili kuondoa tofauti ya pointi na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu