Yanga yahoji kutoshirikishwa mabadiliko ya ratiba Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2019
Yanga yahoji kutoshirikishwa mabadiliko ya ratiba Ligi Kuu

Uongozi wa Yanga umeishushia lawama Bodi ya Ligi kwa kufanya mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu bila ya kuvishirikisha vilabu husika

Juzi Bodi ya Ligi iliurudisha nyuma kwa siku moja mchezo kati ya Yanga dhidi ya JKT Tanzania ambao awali ulikuwa upigwe Jumamosi na kuurudisha siku ya Ijumaa yaani kesho Novemba 22

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Bodi ya Ligi haivitendei haki vilabu kwa kubadilisha ratiba bila ya kuvishirikisha

"Viongozi wa mpira ni wao lakini sisi ndio wadau wakubwa, wanapobadili ratiba ni lazima wafanye mawasiliano na klabu maana sisi ndio tunaocheza sio wao," amesema

"Haiwezekani wanabadili ratiba bila kuhushisha vilabu kwanza ambavyo ndio wadau wakubwa na ndio wenye mechi"

Mabadiliko hayo ya ratiba yaliyofanywa huenda yakawakosesha nafasi ya kushiriki mchezo huo nyota wa Yanga waliokuwa timu za Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’