Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mwana Samatta amekuwa akilaumiwa mchango wake ni mdogo anapoitumikia timu ya Taifa
Nyota huyo anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, ameshushiwa lawama baada ya Stars kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Libya juzi
Licha ya kufunga bao pekee la Stars kwa mkwaju wa penati, Samatta hakuwa na mchezo mzuri jambo lililowakera mashabiki wengi
Hata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Guinea ya Ikweta ambao ulipigwa uwanja wa Taifa, Samatta alikosa nafasi kadhaa za wazi
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Samatta amekubali ukosoaji huo huku akiahidi kufanyia kazi changamoto zote zinazoainishwa na mashabiki

Samatta ni mchezaji wa kutegemewa KRC Genk akiifungia timu hiyo mabao mawili kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu huu