Baada ya kuwa na mwanzo mzuri Yanga, Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Mkwasa huenda akainoa timu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu
Wakati akitangaza kuvunja benchi la ufundi mapema mwezi huu, Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alisema Mkwasa angeiongoza Yanga katika muda wa mpito kabla ya kumpata kocha mpya
Lakini tangu akabidhiwe majukumu hayo, timu imeonekana kubadilika jambo ambalo limewafanya mabosi wa Yanga wasitishe kwa muda mchakato wa kusaka kocha mpya
Mkwasa ameendelea na mipango ya kuimarisha timu ikiwa ni pamoja na kupendekeza maboresho yanayotakiwa kufanywa wakati wa usajili wa dirisha dogo
Hata hivyo matokeo mazuri ndio yatakayo-muhakikishia kupewa mkataba wa kudumu
ADVERTISE HERE