Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Etienne Ndayiragije amesema timu yake ina changamoto upande wa beki wa kulia licha ya mabeki waliopo kujitahidi
Ndayiragije aliwaita Hassan Kessy na Salum Kimenya kwenye kikosi chake kilichoshiriki mechi mbili za kusaka tiketi ya michuano ya Afcon 2021 dhidi ya Guinea ya Ikweta na Libya
Lakini amekiri katika nafasi hiyo, alipenda zaidi kupata beki mwenye uwezo kama Paulo Godfrey 'Boxer' au Shomari Kapombe ambaye hivi karibuni alitangaza kustaafu kuchezea timu ya Taifa
Boxer amekuwa nje kwa takribani miezi mitatu sasa akiuguza majeraha aliyopata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers jijini Dar es salaam na baadae kwenda kujitonesha zaidi kule Botswana
Kabla ya Zahera kutimuliwa Yanga aliwahi kuhoji sababu inayopelekea beki huyo kuwa nje kwa muda mrefu licha ya kuonekana majeraha yake yalikuwa ya kawaida
Hivi karibuni Yanga ilitangaza kuvunja benchi lake la ufundi ikiwa ni pamoja na kumuondoa Dk Edward Bavu ambaye alikuwa daktari wa timu
Kwa sasa nafasi yake inashikiliwa na Dk Sheki Mgazija