Mshambuliaji kinda Maybin Kalengo amerejea kwao kuuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia kuvunjika mguu jijini Mwanza
Kalengo aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba Fc, alifanyiwa upasuaji Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam
Inaelezwa uongozi wa Yanga umempa ruhusu arudi kwao wakati akiendelea kupona majeraha hayo yatakayomuweka nje kwa miezi mitatu
Wakati Kalengo akipewa ruhusa hiyo, kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana nae ameomba ruhusu arejee kwao akatibiwe majeraha yanayomsumbua mara kwa mara
Bigirimana hajawa na mwanzo mzuri kwenye kikosi cha Yanga, kwani tangu asajiliwe amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara
ADVERTISE HERE