Niyonzima afunguka ujio wake Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2019
Niyonzima afunguka ujio wake Yanga

Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima,amefunguka kuwa yuko kwenye mazungumzo na viongozi wa klabu ya Yanga ajili ya kukamilisha usajili wake wakati wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 16 mwaka huu.

Niyonzima amesema kuwa ni mapema mno kuweka wazi kuhusu kurudi kwake tena Yanga lakini siku si nyingi kila kitu kitakuwa hadharani na kufafanua kwamba mazungumzo yake na viongozi wa klabu hiyo yanaendelea vyema.

Aidha, Niyonzima ameongeza kuwa licha ya kwamba Yanga wamempandia ndege na kumfuata Kigali lakini pia kuna timu nyingine mbili kutoka Tanzania ambazo nazo yupo nazo kwenye mazungumzo baada ya kuonyesha nia ya kutaka saini yake.

"Kuna viongozi wawili wa Yanga nimekutana nao na tumezungumza, lakini sio hao tu kuna wengine kutoka kwenye klabu za Tanzania wamekuja na tumefanya mazungumzo, kwangu mimi ninachoangalia nani amekubali ninachotaka ili niweze kuitumikia klabu yake," alisema

Niyonzima aliyetua Yanga mwaka 2012, pia aliitumikia Simba kwa misimu miwili kuanzia mwaka 2017

Kwa sasa anakipiga klabu ya AS Kigali ya Rwanda ambako ana mkataba wa miezi sita

Dimba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’