Tanzania imepoteza mchezo ugenini baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Libya katika mchezo uliopigwa nchini Tunisia
Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 18 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Mbwana Samatta
Mkwaju huo ulitolewa na mwamuzi baada ya Simon Msuva kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Hata hivyo Libya ilisawazisha bao hilo kwenye kipindi cha pili kupitia mkwaju wa penati ambao uliibua utata kwani mpira aliodhaniwa kuushika beki Bakari Mwamnyeto, ulimgonga kwenye goti
Baadae Libya wakafanikiwa kuongeza bao la pili hivyo kuweza kuondoka na alama zote tatu
Pamoja na kipigo hicho bado kampeni ya Stars kufuzu Afcon 2021 iko hai kwani Libya watakuja Dar es salaam kucheza mechezo wa pili na Tanzania na wakati huohuo Stars ikiwa bado na michezo mingine dhidi ya Tunisia na Guinea ya Ikweta
Tunisia inaongoza kundi J ikiwa imekusanya alama sita baada ya leo kuichapa Guinea ya Ikweta 1-0
Tanzania na Libya zote zina alama tatu wakati Guinea ya Ikweta inaburuza mkia ikiwa haina pointi