Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi leo kujiandaa na mikikimikiki ya ligi kuu inayotarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki baada ya mapumziko ya kalenda ya michuano ya Kimataifa
Yanga itarajiwa kucheza na JKT Tanzania Jumamosi, katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru
Yanga inayonolewa na kocha wa muda Charles Mkwasa itaendelea na mazoezi yake kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam
Mazoezi hayo yanatarajiwa kuanza saa tisa Alasiri
Moja ya mabadiliko aliyofanya Mkwasa ni kubadili muda wa mazoezi kutoka asubuhi kwenda Alasiri/jioni
ADVERTISE HERE