Suala la uwanja wa mazoezi liwe kipaumbele

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
18 Nov 2019
Suala la uwanja wa mazoezi liwe kipaumbele

Bado jitihada zinafanyika na uongozi wa Yanga katika kuhakikisha timu inakuwa na kiwanja cha mazoezi

Juhudi zimeonekana kwenye kufanya maboresho uwanja wa Kaunda

Changamoto iliyopo ni athari ya mvua ambayo mara kwa mara imesababisha mafuriko na kurudisha nyuma mipango

Lakini Wanayanga wameendelea kujitolea kumwaga kifusi lengo likiwa kupandisha juu eneo la uwanja ili kuepukana na athari za mafuriko

Uongozi wa Yanga umeweka mkakati wa kuweka viwanja viwili hapo Kaunda, kimoja cha nyasi asili na kingine cha nyasi bandia

Mvua zimekuwa zikichelewesha mchakato lakini mipango iliyopo, hadi kufikia mwezi wa pili, pengine moja ya viwanja hivyo vinaweza kuwa tayari

Jambo la msingi uongozi unapaswa kufanya tathmini ya gharama za ukarabati huo kwani tayari kuna eneo Kigamboni ambalo linaweza kutumia gharama ndogo zaidi

Pamoja na uongozi kuweka malengo ya muda mrefu katika eneo hilo, wanaweza kubadili mipango yao kutokana na mahitaji ya wakati wa sasa

Uwanja wa mazoezi inafaa kiwe kipaumbele namba moja kwa sasa, kwani pamoja na kupunguza gharama, itaisaidia Yanga kufanya program zake za mazoezi bila bugudha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
56m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’