Mkwasa ataka timu ijenge mashambulizi kutoka nyuma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Nov 2019
Mkwasa ataka timu ijenge mashambulizi kutoka nyuma

Kikosi cha Yanga jana licha ya kufanya mazoezi mbalimbali lakini muda mwingi kilifanya mazoezi ya kucheza mpira ambapo Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Mkwasa alionekana kuchagua wachezaji wanaopata nafasi katika kikosi cha kwanza kufanyia kazi mazoezi hayo.

Mkwasa aliwaweka katika timu moja kipa Farouk Shikalo, Juma Abdul, Jaffary Mohammed, Ali Ali, Ally Sonso, Kabamba Tshishimbi, Mo Banka, Mapinduzi Balama, David Molinga, Sadney Urikhob na Mrisho Ngassa.

Baada ya kuwagawa, wakati wote Mkwasa alitaka waanze kujenga mashambulizi kuanzia nyuma wakiwatumia walinzi/washambuliaji wa pembeni kupeleka mashambulizi haraka mbele

Mkwasa alisema wakati anaingia katika timu aliona wanashindwa kuandaa mashambulizi yao kutoka nyuma na aina ya kushambulia ndio maana wameamua kufanya zoezi hilo ambalo limeanza kuzaa matunda.

"Katika mpira ukiondoa ile kuanza katikati mkiwa mmefunga au kuanza wakati wa mechi au mapumziko muda wote lazima muanzie kucheza kutokea nyuma sasa hilo ndio nimeanza kulijenga katika kikosi changu"

"Tutakuwa na uwezo mkubwa wa kujenga na kuanza mashambuliazi kutokea nyuma ambayo kama tukiweza kulifanya hili zoezi vizuri hilo litatusaidia kushambulia muda mwingi na kumiliki mpira"

"Wakati nikiwa sijaanza majukumu haya nimekuwa nikizifutilia timu za Ligi Kuu na kubaini mapungufu yao," alisema Mkwasa ambaye amewahakikishia mashabiki kuwa timu hiyo itakuwa vizuri na kuanza kupachika mabao.

Mkwasa analazimika kubadili mbinu za kikosi chake ambacho wakati kilipokuwa chini ya Mwinyi Zahera kilikuwa kikicheza tofauti

Zahera alipendelea zaidi mchezo wa kushambulia na kujilinda pamoja 'toto-football' huku wakati mwingine akitumia mipira mirefu kupeleka mashambulizi kwa timu pinzani

Aina ya mfumo huo uliwakwaza baadhi ya mashabiki kwani uliondoa ule utamaduni wa Yanga kumiliki mpira, utamaduni ambao Mkwasa anajaribu kuurejesha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’