Siku ya kesho Jumapili, Novemba 17 mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga watakuwa uwanja wa Taifa kupimana ubavu na Coastal Union katika mchezo wa kirafiki
Viingilio vya mchezo huo VIP ni Tsh 5,000/- wakati Mzunguuko ni Tsh 3,000/-
Kaimu kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema atatumia mchezo huo kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao hawakushiriki mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ndanda Fc kutokana na sababu mbalimbali
Mkwasa bado anaendelea kuijenga timu yake
ADVERTISE HERE