Jina la Nicola Kavazovic ni miongoni mwa majina ya makocha wanaotajwa kuwa na uwezekano wa kumrithi kocha Mwinyi Zahera ambaye wiki iliyopita aliondolewa pamoja na benchi lote la ufundi
Kavazovic ni raia wa Serbia mwenye leseni ya UEFA, amefanya kazi katika vilabu mbalimbali barani Afrika
Kavazovic ndiye aliyekuwa kocha wa Township Rollers ambayo iliiondosha Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu wa 2017/18
Ni kile kikosi cha Rollers ambacho kilikuwa kikipiga pasi 'kama zote'
Msimu huo (2017/18) aliiwezesha Rollers kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo
Baadae aliondoka Rollers na kujiunga na AFC Leopards ambayo aliifundisha kwa muda mfupi kabla ya kutimkia Afrika Kusini kwenda kuionoa Free State Stars
Jina la mbabe huyu inaelezwa liko mezani kwa Dk Msolla Mwenyekiti wa Yanga na jopo lake wakiendelea na mchakato wa kumpata mrithi wa Zahera