Beki mpya wa Yanga aliyesajiliwa kutoka Azam FC, Gadiel Michael amesema hakufanya makosa kujiunga na Yanga kwani anaamini ndio timu sahihi itakayomuwezesha kuonyesha uwezo wake na kuonekana mbali zaidi.
Yanga itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu ujao ambapo hata kama itatolewa kwenye raundi ya pili itaungana na Simba kushiriki michuano ya shirikisho.
Kutua kwa Gadiel Yanga kutampunguzia majukumu Haji Mwinyi aliyekuwa analazimika kucheza mechi nyingi kutokana na ushindani mdogo wa namba aliyopata kutoka kwa Oscar Joshua.
Gradiel amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga lakini usajili wake bado haujawekwa waqzi kwa kuwa mkataba wake na Azam FC bado haujamalizika.
Siku chache zilizopita uongozi wa Azam uliibuka na kudai mkataba wa mchezaji huyo utamalizika mwezi Disemba mwaka huu huku Gadiel mwenyewe akidai mkataba wake unamalizika mwezi ujao.

ADVERTISE HERE