Alfred Mtawa ambaye ni Mwanasheria wa beki wa Yanga Andrew Vicent 'Dante',Β amesema hatma ya suala la mteja wake litamalizwa na TFF baada ya pande mbili kushindwa kufikia mwafaka
Dante amekuwa nje ya kikosi cha Yanga tangu kuanza kwa msimu huu akishinikiza alipwe fedha za madai mbalimbali zinazofikia Tsh Milioni 54
Inaelezwa awali TFF ilitoa muda kwa Yanga na Dante kukutana kumaliza sintofahamu iliyopo
Uongozi wa Yanga ulieleza kuwa tayari kumlipa mchezaji huyo kwa awamu, jambo ambalo yeye alilikataa
Mtawa amesema muda waliokuwa wamepewa na TFF kujadiliana umemalizika bila ya mwafaka kufikiwa hivyo wameiachia TFF kufanya uamuzi
Huenda TFF itatumia utaratibu wa kukata mapato ya Yanga katika michezo yake ili kufidia deni la beki huyo kisiki
Hivi karibuni uongozi wa Yanga ulieleza kushangazwa na Dante kuendelea kudai mishahara licha ya kuwa msimu huu hajajiunga na timu
Upo uwezekano mkubwa Yanga itavunja mkataba wake kumruhusu kujiunga na timu nyingine dirisha dogo