Kikosi cha Yanga kimemaliza ziara yake ya mikoa ya Kusini na tayari kimerejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu inayofuata
Aidha kutokana na kusimama kwa ligi kupisha michuano ya Kimataifa, Jumapili ya wiki hii Yanga inatarajiwa kucheza na Coastal Union, ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa ametaka vijana wake wapate mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuivaa JKT Tanzania Novemba 23
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Jumapili watashuka uwanja wa Uhuru kujipima na Coastal Union
Mkwasa atatumia mchezo huo kuwajaribu baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa na timu mkoani Mtwara kutokana na sababu mbalimbali
Aidha atakuwa na nafasi ya kufanyia kazi mapungufu ya kikosi chake kabla ya mchezo wa ligi