Tutampa ushirikiano Mkwasa - Tshishimbi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2019
Tutampa ushirikiano Mkwasa - Tshishimbi

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema wachezaji watampa ushirikiano Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa kwani wanafahamu jukumu lao ni kuhakikisha timu inafikia malengo yake

Tshishimbi amesema mabadiliko ya benchi la ufundi hayawezi kuathiri malengo yao kama wachezaji

"Sisi wachezaji tupo Yanga ni kwa ajili ya kufanya kazi na si vingine. Tutapambana muda wote kuona tunaifanya Yanga kufikia malengo yaliyokusudiwa. Tutampa ushirikiano kocha mpya kama ilivyokuwa kwa kocha aliyeondoka", alisema Tshishimbi

Kulikuwa na hofu kuwa kuondolewa kwa aliyekuwa kocha mkuu Mwinyi Zahera, kungesababisha mgawanyiko miongoni mwa wachezaji

Hata hivyo Tshishimbi ambaye aliteuliwa kuwa nahodha na Zahera akichukua majukumu yaliyoachwa na Ibrahim Ajib aliyetimkia Simba, amebainisha kuwa hakuna kilichobadilika miongoni mwa wachezaji

Kulidhihirisha hilo, chini ya Mkwasa walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda Fc kwenye mchezo wa ligi kuu mkoani Mtwara

Kiwango walichoonyesha katika mchezo huo kiliwafurahisha mashabiki kwani walionyesha mabadiliko makubwa

Waiicheza mpira wa kasi,  wachezaji wakiwa huru kucheza katika maeneo waliyopangwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’