Beki wa Yanga, Haji Mwinyi, amesema Ligi Kuu Bara ipo kwenye hatua ya kupunguzana pointi na inatokana na wachezaji kuwa na hamu ya kujitengenezea ufalme mapema mbele ya mashabiki.
“Kipindi hiki ni cha wachezaji wapya kwa kila timu kuonyesha uwezo wao hadi tone la mwisho, hilo litawasaidia kuwajengea imani kwa mashabiki wao kwamba hawakukosea njia kuwasajili, hilo linapelekea kushindwa kuwa na uimara wa nani anaweza anamudu kukaa kileleni, lakini itafikia wakati wa kujua nani ni nani na nini kitakachovunwa kwa msimu huu,†alisema.
Mchezaji huyo amesisitiza kwamba wao wanajua wanachokifanya, lakini mwisho wa siku hao wapinzani wao walioanza kwa mikwara watanywea tu na Yanga itarudi kwenye nafasi yake ya ubingwa.
Kwa upande wake alisema anaanza kupambana kurejesha heshima ya namba ndani ya kikosi cha kwanza cha kocha Mzambia George Lwandamina na akifanikiwa hilo ndipo atajua afanye jipya gani ndani ya Yanga.
“Anayepata nafasi Yanga anafanya kweli, hii inatusaidia wachezaji kuwa makini uwanjani, naamini nitacheza kwani ligi bado ni mbichi, naendelea kujifunza mapungufu yangu na ubora wangu,†alisema.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE