Nani watapisha haya majembe?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2019
Nani watapisha haya majembe?

Wakati dirisha dogo la usajili likikaribia kufunguliwa, Yanga inahusishwa kuwawania nyota watatu kutoka nchini Rwanda ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake

Nyota hao ni Haruna Niyonzima (Kiungo), Michael Sarpong (Mshambuliaji) na Erick Rutanga (beki-kusoto)

Niyonzima anacheza AS Kigali wakati Sarpong na Rutanga wanacheza Rayon Sports

Kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla na Makamu wake Fredrick Mwakalebela, walibainisha kuwa katika mpango wa kusajili nyota wapya dirisha dogo

"Tumegundua usajili wetu tuliofanya kwenye dirisha kubwa hakututosheleza bado tuna mapungufu, ndio maana tunataka kuziba kwenye dirisha dogo ili tuweze kurudi kwenye mbio za ubingwa msimu huu," ni kauli aliyoitoa Dk Msolla hivi karibuni

Hata hivyo wachezaji wote ni wakigeni, ni wazi Yanga italazimika kuacha nyota watatu wakigeni ili kuzitumia nafasi zao kusajili wapya

Kutegemeana na mikataba yao, baadhi ya wachezaji hasa wale ambao wamekuwa na mchango mdogo wanaweza kupewa mkono wa kwaheri

Habari njema ni kuwa katika mikataba ambayo walisaini, inaelezwa kulikuwa na kipengele cha kupima mwenendo na mchango wao kwenye timu

Mikataba inaweza kupitiwa na kama Yanga haitaridhishwa na kiwango walichoonyesha, wanaweza kuachwa

Pengine kipengele hicho kitaipa ahueni Yanga kulipa pesa nyingi ikitokea inahitaji kuvunja mikataba ya baadhi ya nyota ambao wameshindwa kutamba

Wachezaji 10 wa kigeni waliosajiliwa na Yanga msimu huu ni Farouk Shikhalo, Mustafa Suleyman, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Juma Balinya, Maybin Kalengo na David Molinga

Shikhalo, Lamine, Sibomana, Tshishimbi, Sadney na Molinga hawa wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga kwa maana kwamba wametumika zaidi

Balinya alianza vizuri lakini baadae akapoteza namba katika kikosi cha Zahera jambo ambalo mashabiki walihoji mara kadhaa kwa nini mchezaji huyo hakuwa akipewa nafasi

Mustafa Suleyman na Issa Bigirimana wameshindwa kutamba wakati Kalengo alipata nafasi mara chache lakini majeraha ya kuvunjika mguu aliyopata hivi karibuni yatamfanya akae nje kwa muda mrefu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’